Showing posts with label upambaji. Show all posts
Showing posts with label upambaji. Show all posts

Monday, February 21, 2011

Njano...inavutia



images courtesy of houseandhome

Unaweza kubadilisha rangi ya fanicha kwa kuipaka rangi,kwa mfano rangi ya njano hupendeza.Tumekuwa na mazoea ya kuacha fanicha zote kuwa rangi  ya kahawia  zamu hii badilisha kwa kuzipakaa rangi kama njano hapo juu. Pia unaweza tengeneza sanaa kama kufremu kitambaa ukipendacho matokeo yake hupendeza mfano hapo juu.

Sunday, February 13, 2011

wallpaper ya mistari...

imagevia acupofjo

Wallpapers hupendeza,kama hii ya mistari imetulia pia kwa wale vijana wa kiume ambao hawapendelei rangi za kuwaka hii inapendeza. Pia hiyo ni jinsi nyingine ya kupamba picha za familia na usipendazo ukutani.Enjoy!

Rangi rangi rangi...

image via ohjoy

Tuesday, November 23, 2010

Ramani na watoto





Images via desiretoinspire
Kupamba ni pamoja na kuweka vitu ambavyo vitawaelimisha wanaoishi sehemu husika,kwa mfano ramani kubwa ukutani sio tu inaelimisha bali inapendezesha. Vilevile picha mbali mbali au kufunikia kitambaa kizuri kwenye canvas ni sanaa inayojitosheleza. Watoto wetu nao tusiwasahau,kuwawekea rangi za kuvutia na kuwapangia vizuri na kuwawekea sehemu yao ya kujisomea (picha ya 4 kutoka juu) ni muhimu . Namna hii si tu unawafundisha kuwa wasafi,kuwa na mpangilio na kuwa kujisomea ni muhimu bali pia unawapa ujumbe  pia  unawapa mwelekezo wa vitendo ambao ni muhimu katika maisha yao baadaye.Enjoy!

Friday, November 12, 2010

Vitabu,maua na rangi...



Images courtesy of elleinterior
Shelf ya vitabu,maua mazuri mbalimbali na rangi za kuvutia kama hiyo njano ni mpangilio mzuri hufanya sehemu ivutie na ionekane imetulia.Pia sakafu ya rangi utakayoichagua inapendeza.Muhimu ni kuwa mbunifu na pia kuweka vitu vinakupendezea wewe,vinavyoelimisha au vinavyokukumbusha matukio mbalimbali katika familia yako.Enjoy!

Thursday, November 4, 2010

Pink na picha ukutani...



image courtesy inmyhousedesign.
Rangi ya pink hupendeza ,pia kuweka picha uipendayo ukutano inapendeza na kukufanya ujisikie nyumbani.Enjoy!

Saturday, August 28, 2010

Upambaji wenye mvuto....namna hii

images courtesy bride

Vitu vyenye rangi mbalimbali huongeza mvuto na kuleta mood nzuri ndani ya nyumba.Na kama kawaida macho hayashibi vitu vizuri na vile vile kinachofurahisha macho kinafurahisha moyo pia.Hivyo changanya vitu ulivyonavyo na ongeza rangi mbalimbali uishi pazuri.Enjoy

Wednesday, August 18, 2010

Ufumaji...kutoka Denmark






Images courtesy rice

Kufuma au kuchanganya vitambaa kunapendezesha.Hivi ni kutoka duka liitwalo Rice , Denmark. Kwa kufuma unaweza kupendeza nyumba yako au kufuma kwa ajili ya kumpa mtu zawadi au biashara.Enjoy!